Ni baada ya Kiev kufichua matumizi ya ndege za Kimarekani aina ya F-16 katika vita vyake dhidi ya Russia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, amesema kuwa nchi za Magharibi zinataka kuzidisha vita nchini Ukraine na "zinajitafutia matatizo kwa kufikiria kukidhi maombi ya Ukraine ya kupunguza vikwazo vya matumizi ya silaha zinazoagizwa kutoka nje."
Lovrov ameongeza kuwa, "Wamagharibi ni kama watoto wadogo wanaocheza na njiti za kibiriti, na tunawaambia kwa mara nyingine tena kwamba, kucheza na moto ni jambo hatari sana kwa wale wenye silaha za nyuklia katika nchi za Magharibi."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, vinapozungumziwa Vita vya Tatu vya Dunia, “Wamarekani wanaamini kwamba hili ni jambo litakaloathiri Ulaya pekee iwapo litatokea, Mungu apishe mbali,” akisisitiza kwamba kanuni na nadharia za nyuklia za Russia ziko wazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Rafael Grossi, alionya - jana Jumanne kwamba kukaribia vita kati ya vikosi vya majeshi ya Russia na Ukraine kwenye kinu cha nyuklia cha Kursk ni "hatari sana," kwa sababu vinu vya kituo hicho cha nyuklia viko hatarini.
342/